Swali: Ni ipi njia sahihi ya kuwalea watoto wetu juu ya Tawhiyd na vipi tutawafikishia hilo?

Jibu: Himdi zote ni za Allaah. Walee watoto wako kwa kuhifadhi Qur-aan tukufu, wapeleke katika masomo ya Qur-aan, walee juu ya vitabu vya Tawhiyd na vya ´Aqiydah ambavyo vinasomeshwa kwenye misikiti. Wahifadhishe “Thalaathat-il-Usuwl”, “Qawaa´iyd al-Arbaa´ na “Kashf-ush-Shubuhaat”. Hivi ni vitabu vya msingi. Wasomeshe vilevile Tawhiyd na uwapeleke kwenye Misikiti na katika mizunguko ya darsa na elimu.

  • Mhusika: ´Allaamah ´Abdul-´Aziyz bin ´Abdillaah ar-Raajhiy
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: http://subulsalam.com/play.php?catsmktba=4716
  • Imechapishwa: 17/11/2014