Swalah ya mkusanyiko ya wanawake ni sawa na swalah ya mkusanyiko ya wanamme?

Swali: Je, ubora wa swalah ya mkusanyiko ya wanawake inalingana na ubora wa swalah ya wanamme?

Jibu: Sijui hilo. Allaah ndiye mjuzi zaidi. Kwa sababu swalah ya mkusanyiko wamewekewa katika Shari´ah wanamme. Kuhusu wanawake jepesi linaloweza kusemwa kwao ni kwamba inafaa kwao kuswali swalah ya mkusanyiko. Lakini hawakuamrishwa kuswali swalah ya mkusanyiko. Wameamrishwa kuswali majumbani mwao na hawakuamrishwa kuswali swalah ya mkusanyiko. Lakini hapana vibaya wakiswali swalah ya mkusanyiko na tunataraji kheri katika jambo hilo muda wa kuwa malengo ya mkusanyiko huo ni baadhi wajifunze na kufaidika kutoka kwa wengine, kitu ambacho ni kizuri. Kumepokelewa kutoka kwa Umm Salamah na ´Aaishah ya kwamba waliswalisha baadhi ya wanawake swalah ya mkusanyiko kwa ajili ya kuwafunza na kuwaelekeza. Hapana neno na hapana vibaya kufanya hivo. Kusema kwamba anapata fadhilah za swalah ya mkusanyiko ambayo Allaah amewaahidi wanamme sijui jambo hilo.

  • Mhusika: Imaam ´Abdul-´Aziyz bin ´Abdillaah bin Baaz
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: https://binbaz.org.sa/fatwas/18637/فضل-جماعة-النساء
  • Imechapishwa: 23/03/2023