Usipekui makadirio – utapagawa tu na kuchanganyikiwa

Swali: Ambaye anajiliwa na mashaka kuhusu mipango na makadirio na mambo mengine ya ´Aqiydah. Anachukia jambo hilo na anahisi vibaya. Je, anakuwa miongoni mwa wapotofu na anapata dhambi?

Jibu: Mosi mipango na makadirio ni siri ya Allaah. Kwa ajili hiyo usiingie ndani ya mambo hayo. Usiingie ndani ya mambo hayo. Ni lazima kwako kuamini jambo hilo. Usiingie ndani yake na ukaanza kuhoji hili na lile. Achana na jambo hilo na jisalimishe kwa Allaah (´Azza wa Jall). Jisalimishe kwa Allaah na uamini kuwa yale aliyokadiria ni lazima yawepo, yale aliyoyapanga ni lazima yatokee, kwamba Allaah haumbi kitu pasi na malengo, kwamba Allaah ni Mwenye hekima na anayatia mambo mahali pake na kwamba Allaah hamdhulumu yeyote. Jisalimishe kwa Allaah. Usiingie ndani ya mabishano ya makadirio. Hutofikia chochote kamwe. Utapagawa tu na kuchanganyikiwa. Inatosha tu kuamini mipango na makadirio na ujisalimishe kwa Allaah (´Azza wa Jall). Hili linakutosha.

Kuhusiana na mambo ya shubuha ili uziepuke na uzisome ili uweze kuziepuka, ni jambo linalotakikana kwa muumini. Anapaswa kujua shari ili aweze kujiepusha nayo.

Usijaribu kabisa kuingia ndani ya mipango na makadirio. Kadiri utakavyozidi kuingia ndani ndivo utavyozidi kuwa mjinga zaidi. Kwa nini? Kwa sababu ni siri ya Allaah kwa viumbe Wake. Allaah hakukulazimisha upekue mipango na makadirio. Amekulazimisha ufanye matendo na amemuwezesha kufanya matendo na akakupa uwezo wa hilo. Tenda matendo! Ama kujishughulisha na mipango na makadirio hakukunufaishi kitu. Hili mwachie Allaah (Subhaanahu wa Ta´ala). Wewe fanya kile unachokiweza na achana na yale usiyoyawez. Hili ndio jukumu lako. Unatakiwa kujiepusha na shari na ufanye kheri. Hili ndio jukumu lako.

  • Mhusika: Imaam Swaalih bin Fawzaan al-Fawzaan
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: http://www.alfawzan.af.org.sa/sites/default/files/eg–14041434.mp3
  • Imechapishwa: 23/03/2023