Swali: Je, inafaa kumlipia deni la Ramadhaan mmoja katika ndugu zetu ambaye amekufa na anadaiwa baadhi ya siku za mwezi wa Ramadhaan? Ni nani ambaye atamfungia katika jamaa zake?

Jibu: Wakimfungia wanalipwa thawabu. (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam):

“Mwenye kufa na anadaiwa swawm basi atafungiwa na walii wake.”

Walii ni ndugu na jamaa. Kwa maana nyingine anafungiwa na jamaa zake. Wao ndio wana haki zaidi kuliko wengine. Hapana vibaya pia akifungiwa na wengine. Swawm hiyo inasihi kama deni. Kwa sababu Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) ameifananisha swawm na deni. Inafaa kwa deni likalipwa na ndugu na asiyekuwa ndugu. Hapa ni pale ambapo maiti amelazimika kulipa.

Lakini ikiwa mgonjwa amekufa ndani ya maradhi, hakuendelea kuishi baada ya maradhi na akafa ndani ya ugonjwa wake, hakuna kinachomlazimu.

  • Mhusika: Imaam ´Abdul-´Aziyz bin ´Abdillaah bin Baaz
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: https://binbaz.org.sa/fatwas/2926/حكم-قضاء-الصوم-عمن-مات-وعليه-صوم
  • Imechapishwa: 23/03/2023