Swalah ambayo mtu ametumia Siwaak

Swali: Nini maana ya Hadiyth isemayo:

“Rak´ah mbili kwa kutumia Siwaak ni bora kuliko Rak´ah sabini pasi na kutumia Siwaak.”?

Jibu: Kutumia Siwaak kunapendeza wakati mtu anataka kuswali na wakati wa kutawadha. Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) amesema:

Siwaak inasafisha mdomo na inamridhisha Mola.”[1]

Ameipokea an-Nasaa´iy kwa cheni ya wapokezi Swahiyh kutoka kwa ´Aaishah (Radhiya Allaahu ´anhaa).

Amesema (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) tena:

“Lau nisingechelea kuwatia uzito ummah wangu basi ningeliwaamrisha kutumia Siwaak wakati wa kila swalah.”[2]

Kuna maafikiano juu ya usahihi wake.

Imekuja katika tamko lingine:

“Lau nisingechelea kuwatia uzito ummah wangu basi ningeliwaamrisha kutumia Siwaak wakati wa kila wudhuu´.”[3]

Ameipokea Imaam an-Nasaa´iy kwa cheni ya wapokezi Swahiyh.

Kuhusu Hadiyth isemayo:

“Swalah ambayo mtu ametumia Siwaak ni bora kuliko swalah ambayo mtu hakutumia Siwaak.

ni dhaifu na si Swahiyh. Yaliyopo katika Hadiyth Swahiyh yanatosheleza kutoihitajia.

[1] an-Nasaa´iy (05).

[2] al-Bukhaariy (887) na Muslim (252).

[3] an-Nasaa´iy (02/30430).

  • Mhusika: Imaam ´Abdul-´Aziyz bin ´Abdillaah bin Baaz
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Majmuu´-ul-Fataawaa (26/29) https://binbaz.org.sa/fatwas/20197/فضل-السواك
  • Imechapishwa: 23/03/2023