Swali: Je, inafaa kwa mtu kufunga swawm zinazopendeza kama mfano wa swawm ya siku ya tisa Dhul-Hijjah, swawm ya ´Aashuuraa´ au swawm inayopendeza yoyote ilihali anadaiwa deni la Ramadhaan?

Jibu: Salama zaidi ni yeye aanze kulipa deni na swawm ya faradhi. Hili ndio salama zaidi. Wanazuoni wametofautiana juu ya hilo. Wako ambao wanakataza jambo hilo na wanasema kuwa ni lazima aanze kulipa deni lake, wako wengine wanaona kuwa hapana vibaya na wengine wanasema kwamba akianza kulipa deni lake ndio bora na salama zaidi. Haya ndio maoni yaliyo kati na kati miongoni mwa maoni haya matatu ya kwamba anatakiwa kuanza kulipa deni lake kwa njia ya kuchukua tahadhari zaidi. Baada ya hapo ndio afunge swawm inayopendeza.

  • Mhusika: Imaam ´Abdul-´Aziyz bin ´Abdillaah bin Baaz
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: https://binbaz.org.sa/fatwas/13261/حكم-تقديم-صوم-النوافل-على-صوم-القضاء
  • Imechapishwa: 23/03/2023