Swali: Je, wanawake huswali kwa mkusanyiko?

Jibu: Hapana vibaya wanawake wakiswali kwa mkusanyiko. Hapana vibaya pia wakiswali mmojammoja. Ni jambo zuri endapo wataswali kwa mkusanyiko kwa kutarajia fadhilah za mkusanyiko na kwa lengo la kujifunza. Imepokewa kutoka kwa ´Aaishah na Umm Salamah kwamba waliwaswalisha baadhi ya wanawake kwa mkusanyiko kwa ajili ya mafundisho na mwongozo. Kwa hivyo mwanamke mwenye elimu akiongoza wanawake wengine kwa ajili ya mafundisho, hili ni jambo zuri na wanatarajiwa kupata fadhilah. Hata hivyo swalah ya mkusanyiko sio lazima kwao.

  • Mhusika: Imaam ´Abdul-´Aziyz bin ´Abdillaah bin Baaz
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: https://binbaz.org.sa/fatwas/24896/هل-تستحب-صلاة-النساء-جماعة
  • Imechapishwa: 28/12/2024