Anaenda msikiti wa mbali zaidi licha ya kuwa karibu naye kuna msikiti

Swali:  Vipi ikiwa msikiti uko karibu na nyumba na mtu anaenda msikitini mbali zaidi kwa kutafuta thawabu zaidi?

Jibu: Hakuna tatizo – Allaah akitaka. Hapo ni pale ambapo hakuna madhara yoyote. Lakini ikiwa kitendo hicho kinawazuia wengine kuswali msikitini au kinawadhuru kwa njia fulani, basi ni bora kuswali msikiti wa karibu. Hata hivyo kama hakuna madhara au mtu anaenda msikiti mwingine kwa sababu ya kuhudhuria darsa, kusikiliza usomaji mzuri wa imamu au kwa sababu ya faida inayokubalika katika Shari´ah, basi hapana vibaya.

  • Mhusika: Imaam ´Abdul-´Aziyz bin ´Abdillaah bin Baaz
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: https://binbaz.org.sa/fatwas/24898/حكم-الصلاة-في-المسجد-البعيد-طلبا-للاجر
  • Imechapishwa: 28/12/2024