Swalah ya mkusanyiko inamlazimu kipofu na asiyekuwa kipofu

Swali: Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) hakumpa ruhusa kipofu…

Jibu: Hili ni wakati wa uzito na wakati wa uwepo wa mafuriko. Vinginevyo Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) alimwambia Ibn Umm Maktuum baada ya kumweleza kuwa hana mtu wa kumwongoza njia, akasema:

“Je, wasikia wito wa swalah?” Akajibu: “Ndio.” Ndipo akasema: “Basi imewajibika.”

Swalah ya mkusanyiko inamlazimu kipofu na asiyekuwa kipofu. Hata hivyo hapana neno [kuswali nyumbani] kwa sababu ya udhuru ikiwa kuna matope na utelezi baina yake na msikiti.

  • Mhusika: Imaam ´Abdul-´Aziyz bin ´Abdillaah bin Baaz
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: https://binbaz.org.sa/fatwas/23733/الحكمة-من-الرخصة-للمطر-وعدم-الرخصة-للاعمى
  • Imechapishwa: 17/04/2024