21. Sababu ya kumi na saba ya talaka ambayo ni mawakwe kujihusisha katika maisha ya wanandoa

17 – Mara nyingi kujihusisha kunakuwa kutoka upande wa familia ya mke na pengine chanzo ikawa ni mke. Ikawa mwanamke ana mahusiano ya kudumu na mama yake na amefungamana naye daima na anamtegemea katika kila kitu. Mwanamke huyu akawa anapambika na woga na kutokuwa na uwezo wa kubeba yale majukumu ya kindoa. Mara nyingi mwanamke kama huyu mama yake ndiye anakuwa mwenye mamuzi na mwenye kuiongoza nyumba yote. Kwa hivyo msichana wake anamrejea mama yake katika kila kitu. Kwa mtindo huo haifai kuwa ni mke. Bali wala haifai kuwa ni mama kwa watoto wake, kwa sababu watawalea watoto wasiojiamini na wasiokuwa na utu. Kwa sababu mwanamke huyu hajiamini, hamjali mume wake, hamtaki ushauri ilihali yeye ndiye anayestahiki kutoa mawazo na mwenye kumiliki. Lakini yote hayo ameyatupilia mbali. Mwanamke kama huyu anastahiki kupewa talaka.

  • Mhusika: Shaykh Jamaal bin Furahyaan al-Haarithiy
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: at-Twalaaq – asbaabuhu wa ´ilaajuh, uk. 35-36
  • Imechapishwa: 17/04/2024