Kuswali swalah ya kujitolea kwa mkusanyiko

Swali: Je, inafaa kila swalah inayopendeza kuiswali kwa mkusanyiko?

Jibu: Ni kama mfano wa Dhuhaa na mfano wa swalah ya Tahajjud usiku. Zote hapana vibaya mtu kuziswali kwa mkusanyiko katika baadhi ya wakati. Sio Rawaatib.

Swali: Vipi swalah nyenginezo za kujitolea ikiwa ni kwa lengo la kuwafunza familia?

Jibu: Sijafikiwa na chochote. Rawaatib aziswali kama zilivyo.

Swali: Je, inafaa kuswali pamoja na familia kwa lengo la kuwafunza familia?

Jibu: Hakuna neno kwa lengo la kuwafunza.

  • Mhusika: Imaam ´Abdul-´Aziyz bin ´Abdillaah bin Baaz
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: https://binbaz.org.sa/fatwas/23734/هل-تجوز-صلاة-جميع-النوافل-في-جماعة
  • Imechapishwa: 17/04/2024