Amesema:

وَمَنْ أَعْرَضَ عَن ذِكْرِي فَإِنَّ لَهُ مَعِيشَةً ضَنكًا وَنَحْشُرُهُ يَوْمَ الْقِيَامَةِ أَعْمَىٰ قَالَ رَبِّ لِمَ حَشَرْتَنِي أَعْمَىٰ وَقَدْ كُنتُ بَصِيرًا

”Atakayepuuza ukumbusho Wangu, basi hakika atapata maisha ya dhiki na tutamfufua siku ya Qiyaamah hali ya kuwa kipofu. Atasema: “Mola wangu! Mbona Umenifufua kipofu na hali nilikuwa nikiona?”[1]

Katika Aayah nyingine amesema:

لَّقَدْ كُنتَ فِي غَفْلَةٍ مِّنْ هَـٰذَا فَكَشَفْنَا عَنكَ غِطَاءَكَ فَبَصَرُكَ الْيَوْمَ حَدِيدٌ

”Kwa hakika ulikuwa umeghafilika kutokana na haya, basi Tumekuondoshea kifuniko chako basi kuona kwako leo ni kwa ukali.”[2]

Wakauliza ni vipi haya yatakuwa katika maneno yaliyo wazi. Katika Aayah moja anasema kuwa ni kipofu na katika Aayah nyingine kwamba anaona kwa ukali. Hivyo wakaitilia shaka Qur-aan.

Ama Aayah:

رَبِّ لِمَ حَشَرْتَنِي أَعْمَى

“Mola wangu! Mbona Umenifufua kipofu?”

kwa maana ya kwamba hatoona kuwa yuko na hoja.

وَقَدْ كُنتُ بَصِيرًا

”… na ilihali nilikuwa nikiona.”

Bi maana alikuwa akijadili hoja zake. Hiyo ndio tafsiri ya maneno Yake:

فَعَمِيَتْ عَلَيْهِمُ الْأَنبَاءُ يَوْمَئِذٍ

”Basi zitawafichikia khabari Siku hiyo… ”[3]

Bi manaa hoja zao.

Ama Aayah:

فَبَصَرُكَ الْيَوْمَ حَدِيدٌ

”… kuona kwako leo ni kwa ukali.”

hapo ni pale ambapo kafiri atapotoka kwenye kaburi lake, basi macho yake yatakuwa na ukali. Macho yake hayatopepesa mpaka ayaone yale yote aliyokuwa akiyakadhibisha kuhusu kufufuliwa. Hiyo ndio tafsiri ya maneno Yake:

لَّقَدْ كُنتَ فِي غَفْلَةٍ مِّنْ هَـٰذَا فَكَشَفْنَا عَنكَ غِطَاءَكَ فَبَصَرُكَ الْيَوْمَ حَدِيدٌ

”Kwa hakika ulikuwa umeghafilika kutokana na haya, basi Tumekuondoshea kifuniko chako basi kuona kwako leo ni kwa ukali.”

Ataondoshewa kifuniko. Macho yake yatakuwa makali. Hatopepesa macho mpaka ayaone yale yote aliyokuwa akiyapinga kuhusu kufufuliwa. Hiyo ndio tafsiri ya yale waliyokuwa wakiyatilia shaka mazanadiki[4].

[1] 20:124-125

[2] 50:22

[3] 28:66

[4] Ibn ´Aqiyl al-Hanbaliy amesema:

”Imaam Ahmad (Rahimahu Allaah) ameandika kitabu kinachoitwa ”ar-Radd ´alaal-Jahmiyyah waz-Zanaadiqah wal-Qadariyyah.” (al-Aadaab ash-Shar´iyyah (1/274))

Ibn Taymiyyah amesema:

”Kama alivosema Imaam Ahmad katika kitabu chake ”ar-Radd ´alaaz-Zanaadiqah wal-Jahmiyyah.”  (Tafsiyr Suurat-il-Ikhlaasw, uk. 239)

Ibn Kathiyr amesema:

”… na hivo ndivo alivosema Ahmad bin Hanbal katika kitabu ”ar-Radd ´alaal-Jahmiyyah” (Tafsiyr al-Qur-aan al-´Adhwiym (3/304))

Ibn Hajar al-´Asqalaaniy amesema:

”Amesema waziwazi Ahmad katika kitabu “ar-Radd ´alaal-Jahmiyyah.” (Fath-ul-Baariy (13/598))

  • Mhusika: Imaam Ahmad bin Hanbal (afk. 241)
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: ar-Radd ´alaal-Jahmiyyah waz-Zanaadiqah, uk. 90-91
  • Imechapishwa: 17/04/2024