Allaah amesema kuwaambia makafiri:

وَقِيلَ الْيَوْمَ نَنسَاكُمْ كَمَا نَسِيتُمْ لِقَاءَ يَوْمِكُمْ هَـٰذَا

”Kutasemwa: ”Leo Tunakusahauni kama mlivyosahau makutano na Siku yenu hii.”[1]

Katika Aayah nyingine amesema:

لَّا يَضِلُّ رَبِّي وَلَا يَنسَى

”Mola wangu hakosei na wala hasahau.”[2]

Matokeo yake wakaitilia mashaka Qur-aan.

Kuhusu maneno Yake:

لَّا يَضِلُّ رَبِّي وَلَا يَنسَى

”Mola wangu hakosei na wala hasahau.”

maana yake ni kwamba nakuacheni ndani ya Moto kama nyinyi mlivyosahau kuifanyia matendo Siku yenu hii.

Kuhusu maneno Yake:

لَّا يَضِلُّ رَبِّي وَلَا يَنسَى

”Mola wangu hakosei na wala hasahau.”

maana yake hayaondoki katika kumbukumbu Yake na wala hasahau[3].

[1] 45:34

[2] 20:52

[3] Ibn ´Aqiyl al-Hanbaliy amesema:

”Imaam Ahmad (Rahimahu Allaah) ameandika kitabu kinachoitwa ”ar-Radd ´alaal-Jahmiyyah waz-Zanaadiqah wal-Qadariyyah.” (al-Aadaab ash-Shar´iyyah (1/274))

Ibn Taymiyyah amesema:

”Kama alivosema Imaam Ahmad katika kitabu chake ”ar-Radd ´alaaz-Zanaadiqah wal-Jahmiyyah.”  (Tafsiyr Suurat-il-Ikhlaasw, uk. 239)

Ibn Kathiyr amesema:

”… na hivo ndivo alivosema Ahmad bin Hanbal katika kitabu ”ar-Radd ´alaal-Jahmiyyah” (Tafsiyr al-Qur-aan al-´Adhwiym (3/304))

Ibn Hajar al-´Asqalaaniy amesema:

”Amesema waziwazi Ahmad katika kitabu “ar-Radd ´alaal-Jahmiyyah.” (Fath-ul-Baariy (13/598))

  • Mhusika: Imaam Ahmad bin Hanbal (afk. 241)
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: ar-Radd ´alaal-Jahmiyyah waz-Zanaadiqah, uk. 89-90
  • Imechapishwa: 17/04/2024