Amesema kumwambia Ibliys:

إِنَّ عِبَادِي لَيْسَ لَكَ عَلَيْهِمْ سُلْطَانٌ

”Hakika waja wangu huna mamlaka nao.”[1]

Sambamba na Muusa kusema wakati alipomuua mtu:

هَـٰذَا مِنْ عَمَلِ الشَّيْطَانِ

”Hii ni kutokana na kitendo cha shaytwaan!”[2]

Matokeo yake wakaitilia mashaka Qur-aan na wakadai kuwa ni yenye kujigonga.

Kuhusu maneno Yake:

إِنَّ عِبَادِي لَيْسَ لَكَ عَلَيْهِمْ سُلْطَانٌ

”Hakika waja wangu huna mamlaka nao.”

kunakusudiwa waja wa Allaah ambao amewateua kwa ajili ya dini Yake. Shaytwaan hana ufalme juu yao kuwapotosha katika dini yao au katika ´ibaadah ya Mola wao. Ibliys atawafelisha kwa kuwaingiza ndani ya madhambi, kuhusu shirki Ibliys hatoweza kuwapotosha kutokana na dini yao. Kwa sababu Allaah amewateua kwa dini Yake.

Kuhusu maneno yake Muusa (´alayhis-Salaam):

هَـٰذَا مِنْ عَمَلِ الشَّيْطَانِ

”Hii ni kutokana na kitendo cha shaytwaan!”[3]

kunakusudiwa katika upambaji wa shaytwaan, kama alivyompambia Yuusuf, Aadam na Hawwaa, ambao nao ni katika waja wa Allaah maalum walioteuliwa. Hii ndio tafsiri ya yale ambayo wameyatilia mashaka mazanadiki[4].

[1] 15:42

[2] 28:15

[3] 28:15

[4] Ibn ´Aqiyl al-Hanbaliy amesema:

”Imaam Ahmad (Rahimahu Allaah) ameandika kitabu kinachoitwa ”ar-Radd ´alaal-Jahmiyyah waz-Zanaadiqah wal-Qadariyyah.” (al-Aadaab ash-Shar´iyyah (1/274))

Ibn Taymiyyah amesema:

”Kama alivosema Imaam Ahmad katika kitabu chake ”ar-Radd ´alaaz-Zanaadiqah wal-Jahmiyyah.”  (Tafsiyr Suurat-il-Ikhlaasw, uk. 239)

Ibn Kathiyr amesema:

”… na hivo ndivo alivosema Ahmad bin Hanbal katika kitabu ”ar-Radd ´alaal-Jahmiyyah” (Tafsiyr al-Qur-aan al-´Adhwiym (3/304))

Ibn Hajar al-´Asqalaaniy amesema:

”Amesema waziwazi Ahmad katika kitabu “ar-Radd ´alaal-Jahmiyyah.” (Fath-ul-Baariy (13/598))

  • Mhusika: Imaam Ahmad bin Hanbal (afk. 241)
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: ar-Radd ´alaal-Jahmiyyah waz-Zanaadiqah, uk. 88-89
  • Imechapishwa: 17/04/2024