Swali: Ni vipi inaswaliwa swalah baina ya adhaana na iqaamah?

Jibu: Swalah ya ijumaa haina Raatibah kabla yake. Aswali kile kiwango atachoweza kabla yake. Aswali Rak´ah mbili, nne, nane au kumi. Hakuna kikomo maalum. Aswali kile kiasi atachoweza. Kiwango cha chini kabisa ni Rak´ah mbili kabla ya ijumaa. Haina Raatibah kabla yake. Aswali kile kiasi atachoweza. Bora aswali Rak´ah nne [baada yake] kwa Tasliym mbili.

  • Mhusika: Imaam ´Abdul-´Aziyz bin ´Abdillaah bin Baaz
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: https://binbaz.org.sa/fatwas/22578/هل-لصلاة-الجمعة-راتبة-قبلها
  • Imechapishwa: 06/07/2023