21 – Abu Usaamah ametuhadithia, kutoka kwa Jariyr bin Haazim, kutoka kwa Ya´laa bin Hakiym, kutoka kwa Sa´iyd bin Jubayr ambaye ameeleza kuwa Ibn ´Umar amesema:

“Hayaa na imani vimeambatanishwa pamoja; kikiondoka kimoja, basi kinaondoka kingine.”[1]

22 – Ghundur ametuhadithia, kutoka kwa Shu´bah, kutoka kwa Salamah, kutoka kwa Ibraahiym, kutoka kwa ´Alqamah ambaye amesema:

“Kuna mtu mmoja alikuja kwa ´Abdullaah akasema: “Mimi ni muumini.” Ndipo ´Abdullaah akasema: “Sema pia kwamba uko Peponi. Sivyo hivyo, lakini tunamwamini Allaah, Malaika Wake, Vitabu Vyake na Mitume Yake.”[2]

23 – Waky´ ametuhadithia, kutoka kwa al-A´mash, kutoka kwa Abu Waa-il ambaye amesema:

“Bwana mmoja alikuja kwa ´Abdullaah akasema: “Wakati tulipokuwa tunatembea tulikutana na wapanda farasi ambapo tukawauliza: “Ni kina nani nyinyi?” Akasema: “Sisi ni waumini.” Ndipo akasema: “Walitakiwa kusema kuwa ni katika watu wa Peponi.”[3]

24 – Jariyr ametuhadithia, kutoka kwa Mansuur, kutoka kwa Ibraahiym ambaye amesema:

“Mtu mmoja alimuuliza ´Alqamah kama ni muumini. Akajibu: “Nataraji hivo.”

25 – Jariyr ametuhadithia, kutoka kwa Mughiyrah, kutoka kwa Simaak bin Salamah, kutoka kwa ´Abdur-Rahmaan bin ´Iswmah[4] aliyesimulia kuwa ´Aaishah amesema:

“Nyinyi ni waumini – Allaah akitaka.”

[1] Cheni ya wapokezi ni Swahiyh.

[2] Cheni ya wapokezi ni Swahiyh. Salamah ni Ibn Kuhayl. Upokezi unaokuja baada yake pia ni Swahiyh.

[3] Cheni ya wapokezi wake ni kwa mujibu wa sharti za al-Bukhaariy na Muslim. Vivyo hivyo kuhusu cheni ya wapokezi inayofuata. Upokezi huu upo katika ”Kitaab-ul-Iymaan” (122) cha Ibn Abiy Shaybah kupitia njia nyingine kutoka kwa Abu Waaiyl.

[4] Sikuweza kupata wasifu wake.

  • Mhusika: Imaam Abu Bakr ´Abdullaah bin Muhammad bin Abiy Shaybah al-Kuufiy
  • Mfasiri: Firqtunnajia.com
  • Marejeo: Kitaab-ul-Iymaan, uk. 21-22
  • Imechapishwa: 06/07/2023
  • taaliki: Imaam Muhammad Naaswir-ud-Diyn al-Albaaniy