05. Muumini mwenye imani kamilifu zaidi

12 – Ibn ´Uyaynah ametuhadithia, kutoka kwa ´Amr, kutoka kwa Naafiy´ bin Jubayr ambaye amesema:

“Siku ya kuchinja Mtume wa Allaah (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) alimtuma Bishr bin Suhaym al-Ghifaariy kutangaza Minaa: “Hakuna atakayeingia Peponi isipokuwa nafsi iliyoamini.”[1]

13 – Wakiy´ ametuhadithia: Hishaam bin ´Urwah ametueleza, kutoka kwa baba yake ambaye amesema:

“Msighurike na swalah wala swawm ya mtu. Mwenye kutaka afunge, na mwenye kutaka aswali, lakini hana dini yule ambaye hana amana.”

14 – ´Affaan ametuhadithia: Hammaad bin Salamah ametueleza, kutoka kwa Abu Ja´far al-Khatamiy, kutoka kwa baba yake, kutoka kwa babu yake ´Umayr bin Habiyb bin Khumaashah[2] ambaye amesema:

“Imani inaongezeka na kushuka.” Akaulizwa kuongezeka na kushuka kwake ambapo akasema: “Kuzidi kwake ni pale tunapomtaja na kumcha Mola wetu, na kushuka kwake ni pale tunapoghafilika, tukasahau na kupotea.”

15 – Ibn Numayr ametuhadithia, kutoka kwa Sufyaan, kutoka kwa ´Ubaydullaah, kutoka kwa Naafiy´, kutoka kwa Ibn ´Umar ambaye amesema:

“Ee Allaah! Usiniondoshee imani kama Ulivyonipa.”[3]

16 – Yaziyd bin Haaruun ametuhadithia, kutoka kwa al-´Awwaam, kutoka kwa ´Aliy bin Mudrik, kutoka kwa Abu Zur´ah, kutoka kwa Abu Hurayrah ambaye amesema:

“Imani ni safi[4]. Yule mwenye kuzidi imani inamwacha. Yule mwenye kuilaumu nafsi yake na akarejea, imani yake inarejea.”

17 – Hafsw bin Ghiyaath ametuhadithia, kutoka kwa Muhammad bin ´Amr, kutoka kwa Abu Salamah, kutoka kwa Abu Hurayrah ambaye amesimulia kuwa Mtume wa Allaah (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) amsema:

“Muumini mwenye imani kamilifu zaidi ni yule mwenye tabia njema zaidi katika wao.”[5]

18 – Muhammad bin Bishr ametuhadithia: Muhammad bin ´Amr ametueleza, kutoka kwa Abu Salamah, kutoka kwa Abu Hurayrah ambaye amesimulia kuwa Mtume wa Allaah (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) amesema:

“Muumini mwenye imani kamilifu zaidi ni yule mwenye tabia njema zaidi katika wao.”

19 – Hafsw ametuhadithia, kutoka kwa Khaalid, kutoka kwa Abu Qilaabah, kutoka kwa´Aaishah ambaye amesimulia kuwa Mtume wa Allaah (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) amesema:

“Muumini mwenye imani kamilifu zaidi ni yule mwenye tabia njema zaidi katika wao.”

20 – Abu ´Abdir-Rahmaan al-Muqri’ ametuhadithia, kutoka kwa Sa´iyd bin Abiy Ayyuub, kutoka kwa Ibn ´Ajlaan, kutoka kwa al-Qa´qa´, kutoka kwa Abu Swaalih, kutoka kwa Abu Hurayrah aliyesimulia kuwa Mtume wa Allaah (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) amesema:

“Muumini mwenye imani kamilifu zaidi ni yule mwenye tabia njema zaidi katika wao.”

[1] Swahiyh. al-Bukhaariy, Muslim na wengine wameipokea kwa cheni ya wapokezi yenye kuungana kupitia kwa Ibn Mas´uud na wengineo.

[2] Alikuwa mmoja katika wale Maswahabah waliokula kiapo chini ya Mti. Hana mapokezi, lakini mtoto wake… Jina lake ni Yaziyd bin ´Umar. Sikupata wasifu wake.

[3] Cheni ya wapokezi ni Swahiyh. Vivyo hivyo upokezi unaokuja baada yake.

[4] Bi maana imejitenga mbali na maasi.

[5] Swahiyh. Cheni ya wapokezi ni nzuri. Vivyo hivyo kuhusu upokezi unaokuja baada yake ambao umesahihishwa na at-Tirmidhiy na Ibn Hibbaan ambaye ameipokea kupitia njia nyingine kutoka kwa Abu Hurayrah. Itakuja baada ya Hadiyth ya ´Aaishah na cheni yake ni bora zaidi kuliko hii.

  • Mhusika: Imaam Abu Bakr ´Abdullaah bin Muhammad bin Abiy Shaybah al-Kuufiy
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Kitaab-ul-Iymaan, uk. 19-21
  • Imechapishwa: 06/07/2023
  • taaliki: Imaam Muhammad Naaswir-ud-Diyn al-Albaaniy