Lini inafaa kunyanyua mikono wakati wa du´aa na lini haifai

Swali: Je, ni jambo limewekwa katika Shari´ah wakati wa kuomba du´aa?

Jibu: Miongoni mwa sababu za kuitikiwa du´aa ni kunyanyua mikono wakati wa kuomba du´aa. Ni mamoja wakati anaomba katika Qunuut au maeneo mengine. Isipokuwa yale maeneo ambayo Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) hakunyanyua mikono ndani yake. Miongoni mwa maeneo hayo ni baada ya kumaliza swalah ya faradhi. Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) hakunyanyua mkono maeneo hayo. Sehemu nyingine ni kati ya sijda mbili wala mwishoni mwa swalah. Akiomba du´aa kabla ya kumaliza swalah asinyanyue mikono kwa sababu Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) hakunyanyua mikono. Mtu asinyanyua mikono katika maeneo haya ambayo Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) hakunyanyua. Maeneo mengine ni katika Khutbah ya ijumaa na Khutbah ya ´iyd. Isipokuwa tu wakati ambapo imamu ataomba du´aa ya kunyesha mvua hapo ndipo inafaa kwake kunyanyua mikono.

  • Mhusika: Imaam ´Abdul-´Aziyz bin ´Abdillaah bin Baaz
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: https://binbaz.org.sa/fatwas/22579/متى-يشرع-رفع-اليدين-في-الدعاء
  • Imechapishwa: 06/07/2023