Swali: Je, inajuzu kwa msafiri kukusanya ´Aswr pamoja na ijumaa?

Jibu: Haijuzu. Swalah ya ijumaa haikusanywi na swalah nyingine yoyote. Kwa hivyo aswali swalah ya ijumaa kivyake na aswali ´Aswr ndani ya wakati wake Rak´ah mbili.

  • Mhusika: ´Allaamah ´Abdul-´Aziyz bin ´Abdillaah ar-Raajihiy
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Fataawaa Mutanawwi´ah (21)
  • Imechapishwa: 03/09/2021