Swali: Nilipewa zawadi ya nguo ilio na msalaba ambapo nikaswali hali ya kuwa nimeivaa. Je, niirudie swalah yangu au hakuna kitu juu yangu?

Jibu: Swalah ni sahihi. Lakini aache kivazi hicho, afute msalaba huo au auoshe kwa kitu.

Swali: Ni haramu kuvaa nguo ilio na msalaba?

Jibu: Ndio. Vivyo hivyo kuhusu picha zenye viumbe wenye roho. Isipokuwa zikiharibiwa. Katika hali hiyo hapana vibaya.

Swali: Vipi kuhusu watoto wadogo?

Jibu: Hata watoto wadogo. Kwa sababu picha hiyo inatundikwa na kuhifadhiwa.

  • Mhusika: Imaam ´Abdul-´Aziyz bin ´Abdillaah bin Baaz
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: https://binbaz.org.sa/fatwas/22916/ما-حكم-الصلاة-في-ثوب-عليه-صليب
  • Imechapishwa: 13/09/2023