Kuswali Sunnah baada ya kukimiwa swalah ya faradhi

Swali: Baadhi ya wanazuoni wanasema kuwa akishaanza kuswali swalah inayopendeza na kukakimiwa swalah basi aikamilishe haraka, kwa sababu Allaah (´Azza wa Jall) amesema:

وَلَا تُبْطِلُوا أَعْمَالَكُمْ

“Wala msibatilishe matendo yenu.” (47:33)

Jibu: Hapana, maoni ya sawa ni kwamba aikate. Amesema (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam):

“Hakuna swalah kwa ambaye anaswali peke yake nyuma ya safu.”

Huku ni kubatilisha kunakokubalika kwa mujibu wa Shari´ah.

Swali: Haijalishi kitu hata kama amesharukuu kutoka katika Rak´ah ya mwisho kwa njia ya kwamba atawahi Takbiyrat-ul-Ihraam na hakukubaki isipokuwa sujuud mbili?

Jibu: Hapana neno ikiwa ameshaingia ndani ya safu baada ya Rukuu´. Kama alivofanya Abu Bakrah alipoinuka kutoka katika Rukuu´ akaingia akajiunga na safu. Ikiwa hajajiunga udhahiri wa Sunnah ni kwamba aikate swalah yake. Amesema (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam):

“Hakuna swalah kwa ambaye anaswali peke yake nyuma ya safu.”

Hakuna kinachovuliwa isipokuwa kisa cha Abu Bakrah.

  • Mhusika: Imaam ´Abdul-´Aziyz bin ´Abdillaah bin Baaz
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: https://binbaz.org.sa/fatwas/22912/حكم-من-ابتدا-النافلة-واقيمت-الصلاة
  • Imechapishwa: 13/09/2023