´Aaishah (Radhiya Allaahu ´anh) amesema:

”Allaah awarehemu wanawake wa Muhaajiruun wa mwanzo. Pindi Allaah alipoteremsha:

وَلْيَضْرِبْنَ بِخُمُرِهِنَّ عَلَىٰ جُيُوبِهِنَّ

“Waangushe shungi zao mpaka vifuani mwao.”

walikata vitambaa vyao na wakavitumia kama shungi.”[1]

Imekuja katika upokezi mwingine:

”Walikata vitambaa vyao kwa pembeni na kuvitumia kama shungi.”

al-Haarith bin al-Haarith al-Ghaamidiy amesema:

”Wakati tulipokuwa Minaa nilimwambia baba yangu: ”Ni kundi gani hili?” Akasema: ”Hawa ni watu waliokusanyikia bwana mmoja aliyeacha dini yake.”Tukaketi chini. Alikuwa ni Mtume wa Allaah (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) ambaye alikuwa anawalingania watu kumpwekesha Allaah pekee na kumwamini. Walikuwa wakimkatalia na kumuudhi. Wakati wa mchana wakati ambapo watu walikuwa wametawanyika kutoka kwake, akamjia mwanamke mmoja ambaye shingo yake ilikuwa wazi ambaye alikuwa analia. Alikuwa amebeba kikombe cha maji na kitambaa. Mwanamke yule akampa nacho ambapo akanywa na kutawadha. Kisha akainua kichwa chake kumtazama na kusema: ”Ee msichana mpendwa! Funika shingo yako. Usiogope juu ya baba yako kuwa atashindwa au kudhalilishwa.” Nikasema: ”Ni nani huyu?” Wakasema: ”Ni msichana wa Zaynab.”[2]

[1] al-Bukhaariy, Abu Daawuud na al-Haakim. Ibn Abiy Haatim amepokea tamko kamilifu zaidi kupitia kwa Swafiyyah bint Shaybah ambaye amesema:

”Wakati tulipokuwa kwa ´Aaishah (Radhiya Allaahu ´anhaa) kulitajwa wanawake wa Quraysh na ubora wao ambapo akasema: ”Hakika wanawake wa Quraysh wana ubora, lakini naapa kwa Allaah mimi sijapatapo kuwaona wanawake bora kuliko wa Answaar katika kukithibitisha Kitabu cha Allaah na kuamini ufunuo. Wakati kulipoteremshwa:

وَلْيَضْرِبْنَ بِخُمُرِهِنَّ عَلَىٰ جُيُوبِهِنَّ

“Waangushe shungi zao mpaka vifuani mwao.”

waume zao wakawasomea walichoteremshiwa. Wanamme wakawasomea wake zao, wasichana zao, dada zao na kila ndugu. Hakuna mwanamke yeyote katika wao ambaye hakukata blanketi yake ili kufunika kichwa chake kwa ajili ya kusadikisha na kuamini yale aliyoteremsha Allaah. Siku ya kufuatia wakaswali swalah ya asuhuhi nyuma ya Mtume wa Allaah (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam). Vichwa vyao vilikuwa vimefunikwa utasema juu ya vichwa vyao kunguru walikuwa wameketi juu.”

Yametajwa na Ibn Kathitr na Haafidhw Ibn Hajar katika ”Fath-ul-Baariy” na ziada ni yake. Katika cheni yake ya wapokezi yuko az-Zinjiy bin Khaalid ambaye jina lake anaitwa Muslim na alikuwa mnyonge. Lakini Ibn Marduuyah ameipokea katika tafsiri yake ya Qur-aan kupitia njia nyingine, kama alivosema az-Zayla´iy katika ”Takhriyj-ul-Kashshaaf”. Hadiyth ni dalili ya wazi juu ya kwamba wanawake waliswali nyuma yake (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) zikiwa wazi nyuso zao.

[2] at-Twabaraaniy katika ”al-Mu´jam al-Kabiyr” na Ibn ´Asaakir katika ”Taariykh Dimashq” ambaye amesema:

”Ameipokea al-Bukhaariy katika ”at-Taariykh al-Kabiyr” na Abu Zur´ah. Hadiyth ni Swahiyh.”

  • Mhusika: Imaam Muhammad Naaswir-ud-Diyn al-Albaaniy
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Jilbaab-ul-Mar-ah al-Muslimah, uk. 78-80
  • Imechapishwa: 13/09/2023