Swalah kwa mwanamke iloharibika mimba yake kabla ya siku thamanini

Swali: Kuna mwanamke mimba yake imeporomoka baada ya takriban miezi miwili na siku kumi. Je, aswali au aache kuswali?

Jibu: Ina maana siku sabini. Hapana, asiache Swalah. Hii ni damu safi na sio nifasi. Damu ya nifasi inaanza siku ya thamanini na moja. Mimba ikiingia katika arubaini ya tatu wakati ambapo mtoto anaanza kuwekwa viungo, wakati huu mimba ikiporomoka na kukaja damu baada yake inakuwa ni nifasi. Damu hii inamfanya yeye kuacha Swalah na Swawm kwa muda wa siku arubaini mpaka ikatike. Ama kabla ya kueneza siku thamanini na moja, yaani katika arubaini ya pili, hii haizingatiwi kuwa ni damu ya nifasi. Ni damu safi. Asichi kwa ajili yake Swalah wala Swawm.

  • Mhusika: Imaam Swaalih bin Fawzaan al-Fawzaan
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Sharh Buluugh al-Maraam (34) http://www.alfawzan.af.org.sa/node/12522
  • Imechapishwa: 19/04/2015