Inafaa kuhifadhi picha kwenye kompyuta?

Swali: Ni ipi hukumu ya kuhifadhi picha kwenye intaneti na mitandao mingine?

Jibu: Kuhifadhi picha haijuzu, ee ndugu! Haijuzu kuhifadhi picha. Bali lililo la wajibu ni kuichana. Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) alisema kumwambia ´Aliy (Radhiya Allaahu ´anhu):

“Usiache picha [sanamu] ila hakikisha umeivunja.”

Isipokuwa tu picha za dharurah ambazo unazihitajia kwa ajili ya mambo yako, kama mfano wa leseni, pasipoti na kadhalika. Mambo ambayo huwezi kuyakosa kutokana na manufaa yako. Picha kama hizi zinahifadhiwa kwa ajili ya dharurah. Ama zingine inapaswa uzichane na usizihifadhi kwa ajili ya kumbukumbu, sanaa na mfano wa mambo kama hayo. Vilevile usizitundike kwenye kuta au kuzihifadhi kwenye sanduku.

  • Mhusika: Imaam Swaalih bin Fawzaan al-Fawzaan
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Sharh Buluugh al-Maraam (34) http://www.alfawzan.af.org.sa/node/12522
  • Imechapishwa: 19/04/2015