Kuwatenganisha wanyama wa ´Aqiyqah

Swali: Nikiwa na mbuzi mbili za kuwachinjia watoto. Inajuzu mmoja nikamchinja sehemu na mwingine kumchinja baadaye sehemu nyingine baada ya takriban siku kumi na tano?

Jibu: Inajuzu kuwatenganisha. Lakini hata hivyo ni jambo linaenda kinyume na ubora. Lililo bora zaidi ni kuwachinja wote kwa pamoja wakati mmoja na sehemu moja. Hili ndio bora zaidi.

  • Mhusika: Imaam Swaalih bin Fawzaan al-Fawzaan
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Sharh Buluugh al-Maraam (34) http://www.alfawzan.af.org.sa/node/12522
  • Imechapishwa: 21/04/2015