Swali: Je, inajuzu kwa mwenye kumuombada du´aa Allaah kusema “Ee Mpenzi (حبيبي), niruzuku!” au “Ee Mpenzi, nipende!” na mfano wa maneno kama hayo?

Jibu: Ndio. Inajuzu kusema “Ee Mpenzi!”. Kwa sababu muumini ni mwenye kumpenda Allaah (Subhanaahu wa Ta´ala):

فَسَوْفَ يَأْتِي اللَّـهُ بِقَوْمٍ يُحِبُّهُمْ وَيُحِبُّونَهُ

”… Allaah ataleta watu [badala yao] atakaowapenda nao watampenda.” (05:54)

Ni sawa kufanya hivo. Huku ni kufanya Tawassul kwa Allaah kupitia mapenzi yako Kwake. Kwa kuwa mapenzi yake Kwake ni ´ibaadah. Hili ni tendo jema. Inajuzu kufanya Tawassul kwa Allaah kwa matendo mema ya mtu.

  • Mhusika: Imaam Swaalih bin Fawzaan al-Fawzaan
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Sharh Buluugh al-Maraam (34) http://www.alfawzan.af.org.sa/node/12522
  • Imechapishwa: 21/04/2015