Hili halinapatikana kwa Ahl-us-Sunnah – linapatikana kwa makhurafi

Swali: Je, katika Uislamu kuna Bid´ah nzuri na Bid´ah mbaya?

Jibu: Hili linapatikana kwa makhurafi. Ama Ahl-us-Sunnah wal-Jamaa´ah hawana Bid´ah nzuri. Kwa kuwa Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) amesema:

“Kila kitakachozushwa ni Bid´ah na kila Bid´ah ni upotevu.”

Hakusema kuwa kuna Bid´ah nzuri na mbaya. Bali (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) amesema kwa jumla:

“… kila Bid´ah ni upotevu.”

Mwenye kusema kuwa kuna Bid´ah nzuri anamraddi Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam).

  • Mhusika: Imaam Swaalih bin Fawzaan al-Fawzaan
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Sharh Buluugh al-Maraam (35) http://www.alfawzan.af.org.sa/sites/default/files/blug–1431-08-08.MP3
  • Imechapishwa: 21/04/2015