Kuzika zaidi ya mtu mmoja kwenye kaburi

Swali: Kipindi cha mwisho tumeona watu wanamzika maiti pamoja na mtoto kwenye kaburi moja. Ni yapi maoni yako kwa hilo? Hilo limepelekea kwa baadhi ya wajinga kuamini kuwa tendo hilo lina fadhila na kwamba maiti haadhibiwi kwa kuzikwa kwake pamoja na mtoto huyu.

Jibu: Hili halijuzu. Haijuzu kwenye kaburi kuzika zaidi ya mtu mmoja isipokuwa wakati wa dharurah. Maiti wakiwa wengi sana na Waislamu wakawa hawana nguvu ya kuchimba kaburi la kila mmoja, watazikwa watu wawili watatu kwenye kaburi moja kama alivyofanya Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam). Katika vita vya Uhud wakati maiti zilikuwa nyingi, ikawa kuna uzito kwa Maswahabah kuchimba kaburi kwa kila mmoja, hivyo Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) akaamrisha wazikwe watu wawili watatu kwenye kaburi moja. Alifanya hivi kwa kuwawekea wepesi Waislamu. Ama pasina dharurah haijuzu kuzika kwenye kaburi moja zaidi ya maiti mmoja. Hii ndio Sunnah ya Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) katika kuwazika Maswahabah zake Baqiy´ na kwenginepo. Hakuwa anazika kwenye kaburi moja zaidi ya mtu mmoja.

Kuhusiana na kwamba mtoto atamuombea, huu ni ukhurafi wa wajinga na wapotevu. Ni wajibu kukataza hili. Ikiwa mnajua kuwa hili linafanywa hapa nchini, basi ni wajibu kwenu kuwashtaki watu hawa ili wasitishwe.

  • Mhusika: Imaam Swaalih bin Fawzaan al-Fawzaan
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Sharh Buluugh al-Maraam (34) http://www.alfawzan.af.org.sa/node/12522
  • Imechapishwa: 21/04/2015