Ruqyah haina siku maalum ya kusomwa

Swali: Ruqyah ya Kishari´ah inasomwa mara ngapi? Lini inasomwa; usiku au mchana na ni ipi nyakati bora katika hizo? Je, inasomwa siku ya Ijumaa pekee au katika siku zingine pia za wiki?

Jibu: Ruqyah ya Kishari´ah inasomwa wakati wowote. Itategemea na haja. Haina wakati maalum. Mtu anasomewa pale anapoihitajia. Haina siku maalum, si Ijumaa wala siku nyingine.

  • Mhusika: Imaam Swaalih bin Fawzaan al-Fawzaan
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Sharh Buluugh al-Maraam (35) http://www.alfawzan.af.org.sa/sites/default/files/blug–1431-08-08.MP3
  • Imechapishwa: 21/04/2015