Hii ndio sababu ya kutojuzu kula chakula cha kwenye maulidi

Swali: Je, inajuzu kula nyama iliyochinjwa katika maulidi ya Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam)?

Jibu: Hapana. Hii ni Bid´ah. Hii ni Bid´ah na ni sikukuu iliyozushwa. Vinavyochinjwa katika sikukuu iliyozushwa ni haramu. Vilevile chakula kinachofanywa kwa ajili ya siku hiyo ni haramu. Kwa kuwa hayakufanywa isipokuwa ni kwa ajili ya kuhuisha Bid´ah na kuadhimisha Bid´ah. Haijuzu kushirikiana nao, kula vyakula vyao na wala vichinjwa vyao katika siku hii. Kwa kuwa huku ni kuwashaji´isha, kuwasaidia na kukubaliana nao kwa kitendo hichi kilichozushwa.

  • Mhusika: Imaam Swaalih bin Fawzaan al-Fawzaan
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: http://www.alfawzan.af.org.sa/node/12519
  • Imechapishwa: 19/04/2015