Ni yepi yaliyo wajibu kwa mume juu ya mke wake?

Swali: Kuna mtu amemtaliki mke wake na halafu akamrudi na kumpa pesa kiwango fulani ili kumpoza. Mke wa pili na yeye anaomba pesa kiwango hicho hicho. Je, mke huyu wa pili ana haki ya hilo?

Jibu: Kwa minajili ya kuzuia madhara na kuepuka mizozo ampe kitu kitachomridhisha. Ama kusema ni wajibu sio wajibu. Hakuna lililo la wajibu kwake isipokuwa kupewa matumizi, mavazi, nyumba na makazi. Yanayozidi juu ya haya inakuwa tu ni kwa njia ya kuishi kwa wema na kuboresha ujumba.

  • Mhusika: Imaam Swaalih bin Fawzaan al-Fawzaan
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Sharh Buluugh al-Maraam (13) http://www.alfawzan.af.org.sa/sites/default/files/blug–1430-8-13.mp3
  • Imechapishwa: 19/04/2015