Kuswali Raatibah ya Maghrib na ´Ishaa usiku

Swali: Mwenye kuswali Rak´ah 12 usiku na mchana basi Allaah atamjengea msikiti Peponi…

Jibu: Msikiti au nyumba? Anachomaanisha ni nyumba.

Mwanafunzi: Ameandika msikiti.

al-Fawzaan: Peponi hakuna misikiti wala hakuna kufanya kazi. Allaah atamjengea nyumba na sio msikiti.

Swali: Lau Rak´ah mbili za baada ya Maghrib na ´Ishaa badala yake ataziswali katika swalah ya usiku kitendo hichi kinajuzu?

Jibu: Hapana. Hizi ni Raatibah. Raatibah sio Qiyaam-ul-Layl. Hizi zinafuatana na swalah za faradhi. Rak´ah hizi sio katika Qiyaam-ul-Layl.

  • Mhusika: Imaam Swaalih bin Fawzaan al-Fawzaan
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Sharh Buluugh al-Maraam (13) http://www.alfawzan.af.org.sa/sites/default/files/blug–1430-8-13.mp3
  • Imechapishwa: 19/04/2015