Swali: Je, inajuzu kwa mtu ambaye ameongozwa na Allaah kutaja kisa chake kabla ya kuingia katika Uislamu kwa lengo la kutoa mafunzo? Kwa mfano kama alikuwa ni mlevi au mtumiaji wa madawa ya kulevya kwa ajili ya kutoa maonyo? Je, huku ni kudhihirisha maasi?

Jibu: Sitara inatakikana. Mtu anatakiwa kumsitiri ndugu yake kama jinsi vilevile anavyotakiwa kuisitiri nafsi yake. Asibainishe maasi yaliyompitikia kwa kuwa hii ni fedheha. Hili ni jambo linalofanywa na baadhi ya vijana. Halina msingi. Mtu anapaswa kuisitiri nafsi yake. Allaah amemsitiri. Hivyo basi na yeye anatakiwa kuisitiri nafsi yake kama vile anavyotakiwa kuwasitiri wengine. Sitara ni jambo linalotakikana.

Miongoni mwa masharti ya tawbah sio pamoja na kuwatajia wengine yaliyokupitikia. Hii sio miongoni mwa masharti ya tawbah.

  • Mhusika: Imaam Swaalih bin Fawzaan al-Fawzaan
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Sharh Buluugh al-Maraam (13) http://www.alfawzan.af.org.sa/sites/default/files/blug–1430-8-13.mp3
  • Imechapishwa: 19/04/2015