Mwenye maradhi ya kutokwa hovyo na mkojo anatawadha lini ijumaa?

Swali: Kuna mtu ana maradhi ya kutokwa hovyo na mkono na hivyo anatakiwa kutawadha kila wakati anapotaka kuswali. Ni lini anatakiwa kutawadha kwa ajili ya swalah ya ijumaa?

Jibu: Pale anapotaka kuswali. Atawadhe na kuswali pale kunapokimiwa swalah. Hili ni sawa kwa ajili ya swalah ya ijumaa na swalah zingine.

  • Mhusika: Imaam Swaalih bin Fawzaan al-Fawzaan
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Sharh Buluugh al-Maraam (13) http://www.alfawzan.af.org.sa/sites/default/files/blug–1430-8-13.mp3
  • Imechapishwa: 19/04/2015