Swali: Je, Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) alikuwa akimbusu al-Hasan, al-Husayn na Faatwimah kwenye vichwa vyao au sehemu yoyote usoni? Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) kumsimamia Faatwimah kuna dalili katika tendo hili ya kujuzu kumsimamia mtu mwenye kuingia?

Jibu: Ni sawa kumsimamia kwa ajili ya kumsalimia. Mwenye kuingia unaweza kumsimamia kwa ajili ya kumsalimia. Ama kumsimamia kwa ajili ya kumuheshimu haijuzu.

Kuhusiana na kwamba Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) kumbusu al-Hasan na al-Husayn, mimi sijui lolote kuhusiana na hili.

Kwa hali yoyote kubusiana haiwi midomoni. Hili ni jambo maalum kwa wanandoa. Mbali na wanandoa kubusiana inakuwa kichwani, baina ya macho na kwenye paji la uso.

  • Mhusika: Imaam Swaalih bin Fawzaan al-Fawzaan
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Sharh Buluugh al-Maraam (13) http://www.alfawzan.af.org.sa/sites/default/files/blug–1430-8-13.mp3
  • Imechapishwa: 19/04/2015