Swali: Allaah (Ta´ala) amesema:

إِنَّ اللَّـهَ لَا يَغْفِرُ أَن يُشْرَكَ بِهِ وَيَغْفِرُ مَا دُونَ ذَٰلِكَ لِمَن يَشَاءُ

“Hakika Allaah hasamehi kushirikishwa na anasamehe yaliyo chini ya kwa amtakaye.” (04:48)

Je, ni sahihi kutumia Aayah hii kama dalili juu ya kwamba mwenye kuacha swalah yuko chini ya matakwa ya Allaah, bi maana akitaka atamsamehe na akitaka atamuadhibu?

Jibu: Ee ndugu! Kuna dalili zingine mbali na Aayah hii. Kuna dalili zinazoonesha kufuru ya mwenye kuacha swalah. Vipi utaziacha na kushikamana na Aayah hii? Dalili zinafasiriana, kupeana nguvu na kuonesha ni ipi ambayo ni maalum na ipi siyo maalum. Ni kwa nini unachukua sehemu na unaacha nyingine?

  • Mhusika: Imaam Swaalih bin Fawzaan al-Fawzaan
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Sharh Muqaddimati Ibn Abiy Zayd al-Qayrawaaniy fiyl-´Aqiydah (05) http://www.alfawzan.af.org.sa/sites/default/files/qir–14340106.mp3
  • Imechapishwa: 17/06/2015