Swali: Je, inajuzu kwangu kuwapa Swadaqah wenye kuhitajia ikiwa pato langu nalipata kwa njia ya haramu?

Jibu: Hii sio Swadaqah. Huku ni kujinasua. Jinasue nazo kama mali iliyokupotea isiyokuwa na mmiliki na hawezi kuipata. Zinapewa wenye kuhitajia au michango ya mambo ya kheri ya kijumla. Hata hivyo sio kwa njia ya Swadaqah. Ni kwa njia ya kujinasua.

  • Mhusika: Imaam Swaalih bin Fawzaan al-Fawzaan
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Sharh Muqaddimati Ibn Abiy Zayd al-Qayrawaaniy fiyl-´Aqiydah (05) http://www.alfawzan.af.org.sa/sites/default/files/qir–14340106.mp3
  • Imechapishwa: 17/06/2015