Swali: Muulizaji huyu ni kutoka Albania anasema kuwa katika mji wao kuna pote linaloitwa “Baktwaashiyyah” linalojinasibisha na Uislamu. Wanafanya mambo ya shirki na kufuru; wanachinja kwa ajili ya asiyekuwa Allaah, wanafanya Tawassul kwa wafu na kutabaruku kupitia wao na wanaswali na sisi mara kidogo mno. Vipi tutawachukulia ´Awwaam wao? Je, ni Waislamu na vipi mtu atatangamana na wao?

Jibu: Wabainishieni. Walinganieni katika Uislamu sahihi na muwawekee wazi huenda Allaah akawaongoza. Mimi siwajui na hivyo siwezi kuwahukumu. Lakini wabainishieni na muwalinganie katika Uislamu sahihi na kuwavutia katika Uislamu wa haki huenda Allaah akawaongoza.

  • Mhusika: Imaam Swaalih bin Fawzaan al-Fawzaan
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Sharh Muqaddimati Ibn Abiy Zayd al-Qayrawaaniy fiyl-´Aqiydah (05) http://www.alfawzan.af.org.sa/sites/default/files/qir–14340106.mp3
  • Imechapishwa: 17/06/2015