Swali: Katika kijiji chetu wanachelewesha Swalah ya Ijumaa mpaka robaa saa kabla ya Swalah ya ´Aswr. Hoja yao ni kwamba wanafanya kazi sana. Ninajua kuwa hilo halijuzu, lakini kuna mwanafunzi anayesema Swalah ya Ijumaa kucheleweshwa kiasi hicho ni batili. Je, ni wajibu kwangu kuswali nao Swalah ya Ijumaa au niswali Dhuhr?

Jibu: Swali Ijumaa pamoja nao. Maadamu wanaswali ndani ya wakati, hata kama itakuwa mwishoni, Swalah na wao. Pamoja na hivyo wabainishie kuwa Sunnah ya Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) na Makhaliyfah waongofu na matendo ya Waislamu ni kwamba Swalah ya Ijumaa inaswaliwa mwanzoni mwa wakati. Wabainishie hili.

  • Mhusika: Imaam Swaalih bin Fawzaan al-Fawzaan
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Sharh Muqaddimati Ibn Abiy Zayd al-Qayrawaaniy fiyl-´Aqiydah (05) http://www.alfawzan.af.org.sa/sites/default/files/qir–14340106.mp3
  • Imechapishwa: 17/06/2015