Swali: Mtu anayepuuza swalah, kwa mfano anaswali nyumbani, apewe swadaqah?

Jibu: Apewe swadaqah ingawa kumpa mwingine ndio bora zaidi. Mwingine anayehifadhi swalah ana haki zaidi ya kutendewa wema akiwa anaswali. Ikiwa anaswali nyumbani ni mtenda dhambi. Lakini ikiwa haswali kabisa hapewi zakaah. Apewe kitu kingine isiyokuwa zakaah kwa lengo la kumtia moyo muda wa kuwa ni fakiri sambamba na kumnasihi na kumwelekeza.

Swali: Ni muhitaji na kwa mfano yuko na deni?

Jibu: Akiwa anaswali ni sawa. Apewe, anasihiwe na atiwe adabu. Baraza limtie adabu endapo atakengeuka. Hapa ni pale ambapo ataenda kushatakiwa katika baraza.

  • Mhusika: Imaam ´Abdul-´Aziyz bin ´Abdillaah bin Baaz
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: https://binbaz.org.sa/fatwas/22564/ما-حكم-الصدقة-على-المتهاون-بالصلاة
  • Imechapishwa: 04/07/2023