Swali: Sisi tuko katika jumuiya ya kutoa misaada na tunajiwa na Raafidhwah wengi ambao ni mafukara wanaostahiki kusaidiwa. Je, barua zao zifichwe au wapewe katika swadaqah?

Jibu: Inategemea. Ikiwa ni swadaqah inayopendeza wanaweza kupewa kwa njia ya kuzilainisha nyoyo zao. Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) alikuwa akiwapa makafiri na wengineo. Allaah (Jalla wa ´Alaa) amesema:

لَّا يَنْهَاكُمُ اللَّـهُ عَنِ الَّذِينَ لَمْ يُقَاتِلُوكُمْ فِي الدِّينِ وَلَمْ يُخْرِجُوكُم مِّن دِيَارِكُمْ أَن تَبَرُّوهُمْ وَتُقْسِطُوا إِلَيْهِمْ ۚ إِنَّ اللَّـهَ يُحِبُّ الْمُقْسِطِينَ

”Allaah hakukatazeni kuwafanyia wema na uadilifu wale wasiokupigeni vita katika dini na wala hawakukutoeni kutoka majumbani mwenu – hakika Allaah anapenda wafanyao uadilifu.” (60:08)

Ni sawa kuwapa ikiwa katika kufanya hivo kunazilainisha nyoyo zao na kuwalingania katika Sunnah. Pengine Allaah akawanufaisha kwa sababu hizo.

Swali: Lakini wale wafanyabiashara wao hawatoi.

Jibu: Wapewe isiyokuwa zakaah kwa lengo la kuzilaisha nyoyo zao ikiwa kufanya hivo ni kwa lengo la kuwalingania na kuwapendezeshea Sunnah mara moja moja. Vinginevyo wasipewe na wapewe Ahl-us-Sunnah. Kuhusu zakaah wasipewe.

  • Mhusika: Imaam ´Abdul-´Aziyz bin ´Abdillaah bin Baaz
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: https://binbaz.org.sa/fatwas/22565/حكم-الزكاة-والصدقة-للفقراء-من-الروافض
  • Imechapishwa: 04/07/2023