Sunnah ya kabla ya Maghrib imekokotezwa

Swali: Maneno yake Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam):

“Swalini kabla ya Maghrib Rak´ah mbili kwa anayetaka.”

Aliposema ´kwa anayetaka` alikhofia isije kuwa katika ngazi ya Raatibah?

Jibu: Alichelea wasije kufikiria kuwa ni lazima. Kwa sababu msingi wa amri ni ulazima. Aliposema (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam):

“… kwa anayetaka.”

ikafahamisha kuwa sio lazima na kwamba inapendeza tu.

Swali: Ni lazima?

Jibu: Ni Sunnah iliyokokotezwa na yenye kudumu. Hata hivyo sio ya lazima.

  • Mhusika: Imaam ´Abdul-´Aziyz bin ´Abdillaah bin Baaz
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: https://binbaz.org.sa/fatwas/22566/معنى-صلوا-قبل-المغرب-ركعتين-لمن-شاء
  • Imechapishwa: 04/07/2023