Swali: Ni bora kuswali Sunnah ya ijumaa nyumbani au msikitini?

Jibu: Swalah zinazopendeza zote bora ni kuziswali nyumbani. Lakini hapana vibaya akiziswali msikitini. Zote ni bora kuziswali nyumbani. Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) amesema:

“Swalah bora ya mtu ni nyumbani kwake isipokuwa ya faradhi.”

Swali: Kuna tofauti gani inapokuja katika Sunnah ya ijumaa mtu kuiswali msikitini Rak´ah nne na nyumbani Rak´ah mbili? Je, utofautishaji unasihi?

Jibu: Msingi ni yale aliyoeleza Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam):

“Mwenye kutaka kuswali baada ya ijumaa basi aswali baada yake [Rak´ah] nne.”

Sunnah ni Rak´ah nne. Kamilifu zaidi ni mtu kuswali Rak´ah nne; ni mamoja nyumbani au msikitini. Imekuja katika tamko jingine:

“Mkiswali baada ya ijumaa basi mswali baada yake [Rak´ah] nne.”

Ameipokea Muslim.

Swali: Amri hii inafahamisha kuwa ni lazima?

Jibu: Hapana. Ni kwa yule anayetaka kuswali.

  • Mhusika: Imaam ´Abdul-´Aziyz bin ´Abdillaah bin Baaz
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: https://binbaz.org.sa/fatwas/22571/هل-الافضل-لسنة-الجمعة-البيت-ام-المسجد
  • Imechapishwa: 04/07/2023