Sutrah ya mswaliji baada ya imamu kutoa salamu

Swali: Baada ya imamu kutoa salamu Sutrah ya imamu inabaki kuwa Sutrah ya mswaliji aliyekuja kuchelewa?

Jibu: Hapana. Ikimuwepesikia kuweka Sutrah ni vyema. Vinginevyo akamilishe swalah yake hata kama ni pasi na Sutrah. Pembeni yake akiwa na Sutrah akaiweka mbele yake ni vizuri. Hapo ni pale ambapo atachelea kupita mbele yake mtu. Kwa sababu yuko katika msikiti Mtakatifu mbele yake kuko na Ka´bah na hivyo hahitaji Sutrah. Hili linamuhusu mwanamme na mwanamke wote wawili.

Swali: Hili linahusu Makkah peke yake?

Jibu: Ndio. Ikiwa kuna msongamano na hawezi kuweka Sutrah anasamehewa. Ni mamoja yuko Madiynah au kwengine:

فَاتَّقُوا اللَّـهَ مَا اسْتَطَعْتُمْ

”Mcheni Allaah muwezavyo.”[1]

Swali: Kwa hivyo ni popote?

Jibu: Popote

[1] 64:16

  • Mhusika: Imaam ´Abdul-´Aziyz bin ´Abdillaah bin Baaz
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: https://binbaz.org.sa/fatwas/22272/هل-سترة-الامام-بعد-تسليمه-سترة-للماموم
  • Imechapishwa: 09/03/2023