Swali: Ni yepi maoni sahihi kuhusu Tahiyyat-ul-Masjid baada ya swalah ya ´Aswr?

Jibu: Ni kama nyenginezo. Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) amesema:

“Anapoingia mmoja wenu msikitini basi asiketi chini mpaka aswali kwanza Rak´ah mbili.”

Swali: Lakini baadhi ya watu wanasema kuwa si sahihi.

Jibu: Baadhi ya wanazuoni wanakataza kuswali katika wakati ambao umekatazwa. Lakini maoni ya sawa ni kwamba inafaa. Imeamrishwa daima. Kwa ajili hiyo wakati alipoingia bwana mmoja na imamu alikuwa anatoa Khutbah siku ya ijumaa akamwambia:

“Simama uswali Rak´ah mbili.”

Hapa ilikuwa imamu anatoa Khutbah.

Swali: Akiingia mtu na moja kwa moja akaketi chini anapata dhambi?

Jibu: Afunzwe na aambiwe aswali Rak´ah mbili. Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) alimwamrisha ambaye ameketi kwa kusema:

“Simama uswali Rak´ah mbili.”

Swali: Akikataa?

Jibu: Ukishamfunza Sunnah inatosha. Usimpige.

Swali: Mtu huyu ambaye ameingia siku ya ijumaa na kuketi chini nimwambia asimame?

Jibu: Mwambie asimame. Mwambie ´ee ndugu yangu, Sunnah ni kuswali Rak´ah mbili`.

Swali: Si itakuwa ni kufanya upuuzi?

Jibu: Ikiwa imamu ameshaanza kutoa Khutbah basi muashirie.

Swali: Nimuashirie kwa mkono?

Jibu: Ndio, usizungumze. Lakini Khatwiyb inafaa kwake kuzungumza.

Swali: Ni lazima?

Jibu: Ni Sunnah yenye kukokotezwa.

  • Mhusika: Imaam ´Abdul-´Aziyz bin ´Abdillaah bin Baaz
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: https://binbaz.org.sa/fatwas/22280/حكم-تحية-المسجد-بعد-العصر-وخطبة-الجمعة
  • Imechapishwa: 09/03/2023