Ni kipi bora kutoa swadaqah theluthi ya maji au yote?

Swali: Ni kipi bora kutoa swadaqah theluthi ya maji au yote?

Jibu: Ni lazima abakize kitu kitachomnufaisha na asitoe swadaqah yote. Kama alivosema (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) amesema:

“Jibakizie sehemu katika mali yako ni kheri kwako.”

Atoe swadaqah kile kitachomkuwia chepesi na abakize kitachomsaidia katika kumtii Allaah na awahudumie familia yake.

  • Mhusika: Imaam ´Abdul-´Aziyz bin ´Abdillaah bin Baaz
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: https://binbaz.org.sa/fatwas/22283/هل-الافضل-التصدق-بثلث-المال-ام-به-كله
  • Imechapishwa: 09/03/2023