Sufyaan bin ´Uyaynah aliulizwa:

“Je, imani inazidi na kupungua?”

Akasema:

“Nyinyi hamsomi Qur-aan ambapo ndani yake mna:

فَزَادَهُمْ إِيمَانًا

“Yakawazidishia imani.” (03:173)

Sehemu nyingi. Wakasema “Ndio, tunasema hivi.” Akaulizwa:

“Je, inapugua?”

Bi maana sisi tumekubali kuwa inazidi. Qur-aan imejulisha kuwa inazidi. Inapungua vipi? Akasema:

“Hakuna kitu kinachozidi isipokuwa kinapungua.”

Hii ni dalili za kiakili. Hata hivyo dalili za Kishari´ah katika Sunnah ya Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) zinaonesha kuwa imani inapungua mpaka haibaki isipokuwa sawa na kiasi cha kijipunje kidogo, kama ilivyo katika Hadiyth ya uombezi, Hadiyth ya Anas, Hadiyth ya Abu Sa´iyd, Hadiyth ya Abu Hurayrah (Radhiya Allaahu ´anhum) kuhusu uombezi.

  • Mhusika: ´Allaamah Rabiy´ bin Haadiy al-Madkhaliy
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: adh-Dhariy´ah ilaa Bayaan Maqaaswid Kitaab-ish-Sharï´ah (1/592-593)
  • Imechapishwa: 26/08/2020