Lau kusingelikuwepo dalili nyingine kuwa Allaah anazungumza anayoyataka na pindi Anapotaka zaidi ya dalili hii:

وَكَلَّمَ اللَّـهُ مُوسَىٰ تَكْلِيمًا

“Hakika Allaah alimsemesha Muusa maneno kikweli.” (04:164)

ingelitosha.

Wao – yaani Ahl-ul-Bid´ah – wanasema kuwa ni maneno aliyooyaumba kwenye kiumbe kingine yalio nje ya Allaah – ametakasika Allaah na hilo utakasikaji mkubwa. Ina maana Allaah Hawezi kuzungumza? Je, maneno ni sifa ya upugufu mpaka mumtakase nayo Allaah (Tabaarak wa Ta´ala)? Ububu ambao ni kinyume na maneno na kisichokuwa na uwezo wa kuzungumza ndio aibu. Maneno ni sifa ya ukamilifu. Yule anayezungumza, anayefikisha, anaamrisha na anakataza ni bora kuliko bubu asiyeweza lolote. Ina maa kila anapoelekezwa haleti kheri yoyote. Bubu ambaye Allaah Amempigia mfano katika maneno Yake (Subhaanah):

وَضَرَبَ اللَّـهُ مَثَلًا رَّجُلَيْنِ أَحَدُهُمَا أَبْكَمُ لَا يَقْدِرُ عَلَىٰ شَيْءٍ وَهُوَ كَلٌّ عَلَىٰ مَوْلَاهُ أَيْنَمَا يُوَجِّههُّ لَا يَأْتِ بِخَيْرٍ ۖهَلْ يَسْتَوِي هُوَ وَمَن يَأْمُرُ بِالْعَدْلِ ۙ وَهُوَ عَلَىٰ صِرَاطٍ مُّسْتَقِيمٍ

“Allaah amepiga mfano wa watu wawili; mmoja ni bubu asiye na uwezo juu ya chochote naye ni mzigo kwa bwana wake, popote unapomuelekeza haleti kheri. Je, analingana sawa yeye na yule anayeamrisha uadilifu, naye yuko juu ya njia iliyonyooka.” (61:76)

Je, huyu bubu asiyeweza kuamrisha, kukataza, kujieleza mwenyewe kile anachotaka na mengineyo ndio bora au bora ni yule anayeamrisha uadilifu na akawasaidia watu kwa kuwaamrisha watu yaliyo ya kheri na salama? Pamoja na hayo akawa na nguvu zinazomlinda kwa uadilifu huu.

Kadhalika Allaah anaamrisha uadilifu, wema na Anakataza machafu na maovu (Subhaanahu wa Ta´ala). Vilevile anazungumza, anatuma Mitume, anateremsha vitabu, anaweka Shari´ah na anaumba viumbe kwa maneno Yake (Subhaanahu wa Ta´ala). Wanaposema kuwa Allaah hazungumzi nini maana ya hili? Huku ni kumtukana kwa hali ya juu kabisa. Wao wanachotaka ni kumtakasa na badala yake wakaja kutumbukia katika shari kubwa kuliko hayo waliyoyakimbia.

  • Mhusika: ´Allaamah Rabiy´ bin Haadiy al-Madkhaliy
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: adh-Dhariy´ah ilaa Bayaan Maqaaswid Kitaab-ish-Sharï´ah (1/394-395)
  • Imechapishwa: 26/08/2020