[Aadam akamuuliza Muusa (´alayhimaas-Salaam):]

“Wewe ndiye Muusa uliyesemezwa na Allaah?”

Nukta muhimu hapana ni “Uliyesemezwa na Allaah” bila ya mkati na kati na akasikia Maneno haya. Maneno ni Sifa Yake na haikuumbwa na kujitenga Kwake sehemu nyingine, kama wanavyosema watu wa upotevu. Kadhalika Mu´tazilah na Jahmiyyah wanaosema ya kwamba Allaah mumsemeza Muusa ni kwamba aliumba maneno kwenye mti na Muusa akayasikia. Uhakika ni kwamba Alisikia maneno ya Allaah yenye kutoka kwa Allaah. Kwa ajili hii ndio maana amesema (Subhaanahu wa Ta´ala):

وَكَلَّمَ اللَّـهُ مُوسَىٰ تَكْلِيمًا

“Hakika Allaah alimsemesha Muusa maneno kikweli.” (04:164)

Hii ndio kanuni kwa watu wa sarufi na wa balagha kwamba kule kukazia kunaondosha kuwepo kwa majaaz [mafumbo] na kunathibitisha uhakika. Wao wanasema kuwa maneno ya Allaah ni majaaz. Qur-aan inawakadhibisha na Anasema (Subhaanahu):

وَكَلَّمَ اللَّـهُ مُوسَىٰ تَكْلِيمًا

“Hakika Allaah alimsemesha Muusa maneno kikweli.”

Kauli Yake:

تَكْلِيمًا

“… maneno kikweli.”

Sentesi hii inakazia juu ya kitendo Chake ambacho ni:

وَكَلَّمَ

“Hakika alimsemesha… “

Usisitizo huu unatilia nguvu kitendo chenyewe ambacho ni:

تَكْلِيمًا

“… maneno kikweli.”

ili kuondosha uwepo wa Majaaz. Hili linakubaliwa hata kwa wale vigogo wa Mu´tazilah na wengineo ambao wanaamini Majaaz. Lakini hata hivyo wanatilia kiburi na ukaidi.

  • Mhusika: ´Allaamah Rabiy´ bin Haadiy al-Madkhaliy
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: adh-Dhariy´ah ilaa Bayaan Maqaaswid Kitaab-ish-Sharï´ah (1/393-394)
  • Imechapishwa: 26/08/2020