Ibraahim (´alayhis-Salaam) anaomba azidishiwe imani yake

Ameelezea – Imaam al-Aajurriy – kwa cheni ya wapokezi wake kupitia kwa Sa´iyd bin Jubayr katika kufasiri maneno ya Ibraahiym (´alayhis-Salaam) kuhusu yale Allaah aliyosema juu yake:

وَإِذْ قَالَ إِبْرَاهِيمُ رَبِّ أَرِنِي كَيْفَ تُحْيِي الْمَوْتَىٰ ۖ قَالَ أَوَلَمْ تُؤْمِن ۖ قَالَ بَلَىٰ وَلَـٰكِن لِّيَطْمَئِنَّ قَلْبِي

“Pindi aliposema Ibraahiym: “Mola wangu nionyeshe vipi Unahuisha maiti?” [Allaah] Akasema: “Je, kwani huamini?” Akasema: “La! [Naamini] lakini [kwayo] moyo wangu upate kutulia.” (02:260)

Bi maana mimi ni mwenye kuamini, ewe Mola Wangu. Allaah Anajua kuwa ni mwenye kuamini.

وَلَـٰكِن لِّيَطْمَئِنَّ قَلْبِي

“… lakini [kwayo] moyo wangu upate kutulia.”

Bi maana ili imani yangu iweze kuzidi na kuwa na yakini. Kwa kuwa imani yake inazidi kila siku. Imani yake ni kamilifu lakini hata hivyo inazidi kuwa kamilifu zaidi.

  • Mhusika: ´Allaamah Rabiy´ bin Haadiy al-Madkhaliy
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: adh-Dhariy´ah ilaa Bayaan Maqaaswid Kitaab-ish-Sharï´ah (1/599)
  • Imechapishwa: 26/08/2020